Rais Samia Ahutubia Taifa, Hotuba Maalum Leo Ikulu Dar – Video


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan leo Disemba 8, 2021 amehutubia taifa saa 3 kamili usiku, kuelekea kwenye maadhimisho ya miaka 60 ya Uhuru kesho Desemba 09.

“Ndugu wananchi nawasalimu kwa jina la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, saa chache zijazo tunaadhimisha miaka 60 ya Uhuru wa Tanganyika sasa Tanzania Bara,”

 

“Umuhimu wa siku hii katika historia yetu ni wa kipekee, kwani Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tuliyonayo leo isingeweza kuzaliwa Aprili 26, 1964, kama kusingelitanguliwa na Uhuru wa Tanganyika na baadaye Mapinduzi ya Zanzibar,”

“Miaka 60 ya Uhuru wa Tanzania Bara, imechangia kuleta mafanikio makubwa, ikiwemo kuulinda uhuru wetu na mipaka yake, kujenga umoja wa kitaifa na mshikamano, kuimarisha uchumi wetu na kupunguza umaskini, na kuimarisha demokrasia”

“Kwa mujibu wa takwimu zetu za idadi ya Watu, Watanzania 2,520,559, sawa na asilimia 4.3 ndio waliokuwa wamezaliwa kabla ya Desemba 9, 1961 Hivyo kukosa kwao uzoefu wa hali ya huko nyuma tulikotokea huwawia vigumu kutambua sababu za kujitoa katika makucha ya Ukoloni”

 

“Katika eneo tunalopaswa kujivunia ni kuboresha maisha ya Watanzania na kuongeza upatikanaji wa huduma za jamii na ubora wake, kama sekta ya majisafi, elimu, afya na upatikanaji wa umeme,”

 

“Katika kipindi cha miaka 60 ya uhuru, tumeweza kufikia uchumi wa kati mapema hata kabla ya lengo la kufikia uchumi huo mwaka 2025, hali hii inatuondolea unyonge kimataifa na kutuondolea unyanyapaa.”

 

“Kutokana na kukua kwa Uchumi katika nchi yetu Usafiri wa anga si swala la anasa wala starehe hivyo kufufuliwa au kuimarishwa kwa shirika letu la ndege ATCL ni jambo la lazima” – Rais Samia Suluhu Hassan

“Kwa sasa shirika letu la ndege lina jumla ya ndege 12 na tayari tumefanya malipo ya awali ya ununuzi wa ndege nyingine 5” – Rais Samia Suluhu Hassan

⚫️ SIKILIZA + 255 GLOBAL RADIO LIVE: http://ndstream.net/globalradio/ ⚫️ Kwa UPDATES zote, Download GLOBAL APP: ⚫️ ANDROID:http://bit.ly/38Lluc8 ⚫️ iOS:https://apple.co/38HjiCx


Toa comment