The House of Favourite Newspapers

VIDEO: SpotiHausi –Exclusive Interview na Malimi Busungu & Ivo Mapunda

0
Kutoka kushoto ni Wilbert Molandi, (wandishi wa Championi na mchambuzi wa soka), Philip Nkini (mhariri na mchambuzi), Malimi Busungu (straiker wa Yanga) na Saleh Ally (Mhariri Kiongzoi wa Championi) wakiwa kwenye Studio za Global TV Online baada ya kumalizika Kipindi cha SpotiHausi.

GLOBAL TV Online kupitia kipindi chake cha Michezo cha SpotiHausi kinachoruka hewani kila Alhamsi saa 10:00 jioni leo imeafanikiwa kuwanasa wakali wawili wa soka hapa Bongo ambao ni kipa wa zamani Ivo Mapunda na Straiker wa Yanga, Malimi Busungu.

Akizungumza wakati wa interview hiyo, Ivo Mapunda aliyewahi kuichezea Gor Mahia ya Kenya, Yanga, Simba na Azama amesema kuwa wengi walizani pengine taulo alilokuwa akiingia nalo uwanjani lilikuwa ni kwa ajili ya mambo ya kishirikina, lakini yeye alikuwa akiingia na taulo kwa ajiri ya kufuta jasho mikono.

Kwa upande wake Straiker wa Yanga, Malimi Busungu ambaye hajaonekana uwanjani kwa muda mrefu sasa amekiri kuwa na mtafaruku na uongozi wa kalu hiyo huku akishindwa kueleza ni tatizo lipi limewafanya watofautiane.

 

Mapunda ameeleza kuwa ilifika wakati taulo hilo likamuongezea umaarufu, akajikusanyia mashabiki hadi kufikia hatua ya Kampuni ya SuperSport kumnunulia mataulo zaidi ya 300 ambayo alikuwa akiyatumia uwanjani na baada ya mechi anawagawia mashabiki wake.

Aidha Busungu amewaomba radhi mashabiki na wapenzi wa Yanga kwa kitendo alichokifanya baada ya picha kuvuja hivi karibuni zikimuonesha amejiachia huku akiwa kwenye hali ya kulewa pombe.

TAZAMA FULL INTERVIEW HAPA

Leave A Reply