Rais John Magufuli amesema serikali yake imedhamiria kumaliza tatizo la usafiri wa barabara nchini. Aidha amesema serikali yake haitatoa chakula cha msaada kwa wananchi wazembe ambao hawajitumi kufanya kazi.
Hayo aliyasema wilayani Kakonko wakati wa ziara ya uzinduzi wa ujenzi barabara ya urefu wa kilomita 50 kutoka Nyakanazi hadi Kibondo mkoani Kigoma ambayo itajengwa kwa lami.
Vilevile alisema mara zabuni ikitangazwa, serikali tayari ina fedha za kujenga barabara ya Kasulu-Kibondo kwa kiwango hichohicho.
Alitoa onyo pia kwa makandarasi wazembe akiwataka wafanye kazi kufuatana na mikataba na kwa utaalam unaotakiwa na kwamba serikali iko tayari kuwatimizia mahitaji katika majukumu yao. “Nakuomba waziri, kama kuna pesa mkandarasi anadai, mhakikishe wiki ijayo analipwa na hii lami ianze kujengwa usiku na mchana,” alisisitiza rais.
Akigusia suala la ujambazi sehemu hiyo, Magufuli alimtaka Mkuu wa Mkoa wa Kigoma alishughulikie kwa nguvu zote ili kulikomesha kwa vile, miongoni mwa ukatili unaofanywa na majambazi ni pamoja na kuwatoboa macho wananchi ili kuwazuia wasitoe ushahidi waliouona.
Kuhusu kodi, alisema serikali imefuta kodi 80 kwenye mazao, kodi saba kwenye mifugo na kodi nyingine kwenye uvuvi. Katika suala la chakula alisisitiza kila mtu afanye kazi kwa ajili ya uzalishaji wa chakula chake na nchini kwa jumla.
“Sileti chakula ng’o, asiyefanya kazi na asile, asiiyekula na afe. Mfanye kazi kweli, na huo ndiyo ukweli,” alisisitiza. Akizungumzia uwekezaji katika madini kutoka nje na ndani, Rais Magufuli alisema serikali yake imewaita wawekezaji kutoka nje na iwapo hawatajitokeza mapema migodi yote bora watapewa Watanzania waiendeshe
ALICHOKISEMA RAIS MAGUFULI
#JPMKakonkoKigoma: Tumedhamiria kumaliza tatizo la usafiri wa barabara hapa nchini. Barabara hii tutaitengeneza kwa kiwango cha lami.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Nawaruhusu mtangaze hata wiki ijayo zabuni ya kutengeneza barabara ya Kasulu – Kibondo, pesa tayari ipo. @MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Naomba RC wa Kigoma ulishughulikie suala la ujambazi na watu kutobolewa macho kwa misumari.https://t.co/vPtn2dsQ8z
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Akionekana mtu ambaye ni mgeni na haeleweki, toeni taarifa mapema kuzuia uhalifu usio wa lazima.https://t.co/vPtn2dsQ8z
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Nakuomba Waziri wa Ujenzi na Uchukuzi, @MbarawaM ukiona mkandarasi anazembea, fukuza. Tunataka kazi zifanyike.
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma:Nakuomba Waziri kama kuna pesa mkandarasi anadai,mhakikishe wiki ijayo analipwa na hii lami ianze kujengwa usiku na mchana
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Tumefuta kodi 80 kwenye mazao, kodi 7 kwenye mifugo na kodi nyingine kwenye uvuvi. –@MagufuliJP
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Sileti chakula ng’o, asiyefanya kazi na asile, asiiyekula na afe. Mfanye kazi kweli, na huo ndiyo ukweli. –@MagufuliJP pic.twitter.com/cA2RPISuL3
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
#JPMKakonkoKigoma: Tumewaita hao wawekezaji wa madini waje tuzungumze, wakichelewa tutafunga migodi yote bora tuwape Watanzania –@MagufuliJP pic.twitter.com/MG36DoAaGi
— Global Publishers (@GlobalHabari) July 21, 2017
[…] Chakula hiki kimetengenezwa kitaalamu ili kumfanya mgonjwa apate nafuu, na hapo ndipo huitwa dawa. […]