Luhende Amtisha Tshabalala Simba

BEKI wa pembeni wa Kagera Sugar, David Luhende, amekubali kukaa meza moja na mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya kujiunga na timu hiyo, huku akisema ana uhakika wa namba kwenye kikosi hicho.

 

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu tetesi zizagae za beki huyo anayecheza upande wa kushoto nafasi inayochezwa na Mohammed Hussein ‘Zimbwe’ kutakiwa na Simba.

 

Simba imepanga kukifanyia maboresho kikosi chao katika baadhi ya nafasi ikiwemo ya ulinzi, kiungo na ushambuliaji katika kuelekea msimu ujao wa ligi.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Luhende alisema kuwa yeye ni mchezaji huru ambaye mkataba unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu, hivyo anaruhusiwa kuzungumza na timu nyingine itakayomuhitaji.

 

Luhende alisema kuwa bado viongozi wa Simba hawajamfuata rasmi kwa ajili ya mazungumzo, lakini yeye yupo tayari kujiunga na timu hiyo kama wakifikia muafaka mzuri.Aliongeza kuwa anaamini kiwango chake, hivyo ana uhakika mkubwa wa kuanza kucheza katika kikosi cha timu hiyo.

 

“Mimi maisha yangu yanategemea soka, hivyo nipo tayari kujiunga na timu yoyote itakayonihitaji, lakini kitu kikubwa nitakachokiangalia ni maslahi pekee.

 

Hivyo niikaribishe Simba na timu nyingine itakayohitaji huduma yangu kwa ajili ya kufanya mazungumzo ya awali kabla ya kusaini mkataba kwa makubaliano mazuri, naamini pale Simba mimi naweza kucheza,”alisema Luhende mwenye asisti saba msimu huu.

WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA, Dar

KIDAO AWALIPUA WAGOMBEA URAIS TFF – “TUTAFUNGIWA na FIFA, MALALAMIKO HAYAJENGI”


Toa comment