LULU AJIRI BODIGADI WA KIKE

 MWANAMUZIKI anayetamba na wimbo wa Mapopo ulio hewani kwa sasa, Lulu Abasi ‘Lulu Diva’ baada ya pesa kumtembelea ameajiri bodigadi wa kike tofauti na wanamuziki wengi ambao huwa na mabodigadi wa kiume.

 

Akiongea na Risasi Jumamosi, Lulu alifunguka kuhusu majukumu ya bodigadi wake huyo aliyemtaja kwa jina la Beatrice kuwa ni kuangalia anakula nini, kumchagulia nguo za kuvaa kwenye shoo, kumbebea pochi na kukagua gari lake kabla hajapanda kwa kile alichosema, “ya walimwengu ni mengi”.

 

“Si unajua ya walimwengu ni mengi sana, lazima kabla sijapanda kwenye gari anikagulie na kuangalia kama pako salama, pesa ikiwepo ni kuitumia ipasavyo,” alisema Lulu Diva kwa tambo.

Aidha, Lulu alitaja mshahara anaomlipa bodigadi huyo kuwa ni shilingi milioni moja kila mwezi ambapo ameridhia mwenyewe na wanaelewana kwa kiwango hicho.

 

“Unajua niliamua kumchukua bodigadi wa kike kwa sababu ndio tunaelewana, anaweza kuelewa lugha ninayoongea tofauti na wengine wa kiume kunielewa ingekuwa ngumu,” alisema Lulu.

 

Lulu ni msanii wa muziki aliyeanzia kwenye filamu, baadaye akaingia kwenye kupamba video za wasanii ‘video queen’ kisha akatoboa na kuingia kwenye muziki wa Bongo Fleva ambapo mpaka sasa ameshatoa nyimbo nyingi zinazobamba kitaani kama vile Mapopo, Ona (Rich Mavoko) na Usimwache.


Loading...

Toa comment