The House of Favourite Newspapers

Makonda Abaini Polisi Wanaojihusisha na Unga, Kuvusha Kobe (Video)

0
Paul Makonda akizungumza na wanahabri.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda amesema amewabaini baadhi ya askari polisi jijini humo wanaoshiriki biashara haramu ya dawa za kulevya na wengine wanaoshiriki kuvusha kobe kwenda nje ya nchi.

Hayo ameyasema leo Ijumaa, Agosti 25, 2017 wakati akipokea vifaa kwa ajili ya kusaidia Jeshi la Polisi kutimiza majukumu yake ya kulinda usalama.

“Niliposema kuna askari wanajihusisha na biashara ya madawa wengine mlikataa, kuna baadhi ya polisi tumewabaini, waliitwa na wasamalia wema kwenda kwenye hoteli moja ambapo kulikuwa na wauza madawa, walipofika wakafanikiwa kuwakamata wakaondoka nao.

“Lakini cha ajabu walifika nhiani wakazungumza nao wakapewa kitu kidogo wakaachia wahalifu hao. Wahalifu wakarudi hadi kwenye ile hoteli na kuanza kuwaghasi wahudumu wa pale kuwa wamewachongea, hawa lazima tuwashughulikie” alisema Makonda.

“Wengine nao wanajihusisha na kuvusha wanayama wetu kobe kwenda nje ya nchi, hao nao tutawanyoosha.” aliongeza.

TUKIO LENYEWE LIKO HAPA

Leave A Reply