The House of Favourite Newspapers

Makonda Azindua Viwanda Vidogo Karakana Mwananyamala Dar

0
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, akizindua karakana kwenye viwanda vidogo  Mwananyamala Dar.
…Akisalimiana na wadau mbalimbali baada ya uzinduzi.
…Akiangalia baadhi ya bidhaa kwenye viwanda vidogovidogo vilivyozinduliwa.
Kikundi cha ngoma kikitoa burudani wakati wa uzinduzi huo.⁠⁠⁠⁠
Majengo ya viwanda hivyo yaliyozinduliwa.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, amezitaka manispaa za jijini Dar es Salaam kutengeneza mazingira rafiki kwa wajasiriamali wadogo ili iwe rahisi kwa wao kujiwezesha na kuendelea na miradi mbalimbali.

Makonda amesema kwa kufanya hivyo itawarahisishia wao kuwatambua kwa urahisi pindi watakapojiunga kwenye vikundi ili kujipatia mikopo itakayowasaidia kuongeza nguvu katika biashara zao.

Akizungumza mara baadaya kuweka jiwe la msingi kwenye uzinduzi wa viwanda vidogovidogo vilivyopo Karakana ya Jiji Mwananyamala alisema: “Nawapongeza kwa kazi nzuri mnayoifanya kwa manispaa ya Kinondoni lakini pia kuunga mkono jitihada za wajasiriamali kwa kuwapa mikopo kupitia vikundi vyao, nitoe wito pia kwa watendaji kwamba msitoe mikopo holela kwani itakuwa kazi kuirejesha”.

Aidha amewapongeza pia Halmashauri ya Jiji kwa kuanza kutoa ruzuku kwa manispaa kwani hapo mwanzo walikuwa hawatoi.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo wa ujenzi wa viwanda vidogovidogo kwa Mkuu wa Mkoa, Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam, Sipora Liana, amesema kuwa kupitia mradi huo Jiji la Dar es Salaam limeendelea kutoa kipaumbele kwa wanawake, vijana na walemavu wanaopata mikopo kutoka Halmashauri ya Jiji kwa kuwa mazingira wanayofanyia kazisi rafiki na wanahangaika kupata masoko ya uhakika.

NA DENIS MTIMA/GLOBAL PUBLISHERS LTD

Leave A Reply