×

Mrembo Atoboa Siri Penzi na Kiba

 

MAKUBWA! Wakati kukiwa na wingu zito kuhusu ndoa ya msanii wa Bongo Fleva, Ali Saleh Kiba ‘AliKiba’, membo kutoka nchini Kenya, Bridget Achieng ameibuka na kutoboa kuwa aliwahi kumzimikia kinoma mkali huyo anayetamba na wimbo wa Mshumaa.

 

Mapema jana, mtandao maarufu kwa habari za mastaa nchini Kenya uliporomosha maelezo marefu ya mrembo huyo kwamba alikutana miaka kadhaa iliyopita na Kiba na alimzimikia kwamba ilibaki kidogo tu amkubali awe wake wa maisha.

 

Kwa siku nzima ya jana, picha za mrembo huyo ambaye ni muigizaji nchini mwao zilisambaa kwenye kurasa chache za wambea wa Instagram ambapo kikubwa kilichokuwa kikijadiliwa ni tatuu ya jina la Kiba aliyojichora mkononi.

 

Kwenye mtandao huo, mrembo huyo alimmwagia sifa kibao Kiba kwa kusema ni mwanaume mzuri anayefaa kuwa mume japo yeye ilishindikana.

“Ilishindikana japo tulikuwa marafiki na tumeendelea kuwa marafiki hadi sasa. Ni mwanaume mzuri sana,” alisema mrembo huyo.

 

Mrembo huyo alisema sababu ya kuamua kutoendelea na Kiba ni kitendo cha msanii huyo kuwa na watoto watatu jambo ambalo kwake aliona halimpendezi.

“Mimi nilikuwa nataka mwanaume ambaye hana kabisa watoto nizae naye na wakati huo Kiba alikuwa na watoto watatu tayari,” alisema.

 

Baada ya kupata ubuyu huo wa motomoto, Amani lilijaribu kumvutia waya AliKiba lakini simu yake iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe kumhusu mrembo huyo, hakujibu.

 

Hata hivyo, Amani lilimtafuta mmoja wa mameneja wa msanii huyo, Aidan Seif ambaye aling’aka kuhusu habari hiyo na kusema huenda mrembo huyo ana tatizo la akili.

“Atakuwa na matatizo huyo dada si bure,” alisema Aidan.

 Stori: Mwandishi Wetu, Dar

Leave a Comment