The House of Favourite Newspapers

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA Yatoa Ufafanuzi Taarifa Inayosambaa Mtandaoni

0

 

Mamlaka ya Mapato Tanzania TRA imetoa ufafanuzi juu ya taarifa inayosambaa kwenye mitandao ya kijamii kuhusu malalamiko yaliyotolewa na mfanyabiashara Emmanuel Gadi akihituhumu TRA kutengeneza mfumo wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo halali wa Serikali tangu 2018.

TRA inaufahamisha umma na jamii kwa ujumla kwamba Mamlaka hiyo haina mfumo wowote mwingine inaouendesha wa kuingiza mizigo nchini nje ya mfumo wa Forodha ambao unatumika kwa mujibu wa Sheria ya Usimamizi wa Forodha ya Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Aidha TRA imebaini kuwepo viashiria vya ukwepaji kodi kwani ni dhahiri kuwa mzigo huo uliingizwa kwa njia za magendo. Kupitia taarifa hiyo TRA imemtaka mlalamikaji kuwasilisha nyaraka na uthibitisho wa kampuni yake kuingiza mzigo huo nchini mara moja ili hatua stahiki zichukuliwe.

Leave A Reply