Watu wawili wanadaiwa kufariki dunia baada ya kuliwa na mnyama kiboko katika bwawa la milala Manispaa ya Mpanda mkoa wa Katavi.
Katika tukio hilo, mwili wa Mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la John Osso (32) mkazi wa mtaa wa Milala manispaa ya Mpanda umeopolewa huku mtu mwingine ambaye bado majina yake hayajajulikana na mwili wake haujaonekana.
Kwa mujibu wa mashuhuda wamesema watu hao walikua wakifanya shughuli za uwindaji usiku wa manane katika bwawa hilo.