The House of Favourite Newspapers

Matola: Simba Waisapoti Yanga Kimataifa

Selemani Matola

KOCHA wa Polisi Tanzania, Selemani Matola amefunguka kuwa mashabiki wa timu zote Tanzania ikiwemo Simba wanatakiwa kuzisapoti Yanga na Azam FC kwa kuwa zinawakilisha taifa na kuna faida ya kufanya hivyo.

Kauli hiyo imekuja baada ya Simba kufanya vizuri msimu uliopita kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika kwa kufika hatua ya robo fainali jambo lililosababisha timu nne za Tanzania kushiriki michuano ya kimataifa.

Msimu huu katika mashindano ya kimataifa, iliwakilishwa na Simba, KMC, Azam FC pamoja na Yanga,
Simba na KMC wametolewa tayari huku Yanga itacheza dhidi ya Zesco United ya Zambia kesho Jumamosi huku Azam FC ikiivaa Triangle United, Jumapili katika Uwanja wa Azam Complex, Chamazi.

 

“Unajua Yanga na Azam wanahitaji sapoti kutoka kwa Watanzania hasa wanapocheza hapa nyumbani, tunatakiwa kuwa kitu kimoja na kuweka kando mambo ya Simba, Namungo sijui Mtibwa, tuachane nayo kwanza kwa sasa tuwasapoti wenzetu.

 

“Kama tukisimama kuwaunga mkono Yanga na Azam hii ina faida kwetu kama nchini. Lakini pia wanatakiwa kutumia vizuri viwanja vya nyumbani na kutorudia makosa yale ambayo yalifanywa na Simba na KMC,” alisema Matola.

SPOTI HAUSI: NJIA Za YANGA Kutoa ZESCO UNITED Ni HIZI..!

Comments are closed.