The House of Favourite Newspapers

Mbrazili wa Simba Aanza Kutupia Sauz

STRAIKA mpya wa Simba, Wilker Henrique da Silva, raia wa Brazil, ameanza kuonyesha cheche baada ya jana kutupia bao moja kwenye ushindi wa mabao 4-0, ilioupata klabu yake.

 

Mbrazili huyo alifunga bao hilo moja katika mchezo wa kirafiki ambao Simba walicheza na timu ya Orbret TVET, mechi iliyopigwa Rusternburg, Afrika Kusini ‘Sauz’ ambapo Simba wameweka kambi.

Kikosi hicho cha kocha Patrick Aussems, kilicheza mechi hiyo ikiwa ni ya kwanza tangu walipoenda kuweka kambi nchini Afrika Kusini.

 

Mbali na Mbrazili huyo kufunga, katika mechi hiyo pia straika John Bocco alifunga mabao
mawili, sambamba na kiungo Hassan Dilunga. Kikosi hicho cha Simba pia kesho Alhamisi kitacheza na Platinum Stars iliyo Ligi Kuu Afrika Kusini ikiwa ni sehemu ya mechi za maandalizi ya msimu ujao.

HII ndio GHARAMA ya GARI la Q CHIEF ALILOKABIDHIWA na HARMONIZE

Comments are closed.