The House of Favourite Newspapers

Mbunge wa Singida Apokea Msafara wa Waandishi Wanaokwenda Burundi

Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu (kushoto) akiwapokea Waandishi wa habari za michezo wanaokwenda nchini Burundi kuisapoti timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ .

MBUNGE wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu, ameupokea msafara wa Waandishi wa habari za michezo wanaokwenda nchini Burundi kuisapoti timu ya taifa Tanzania ‘Taifa Stars’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali Kombe la Dunia zitakazofanyika nchini, Qatar.

 

Kingu amesimamisha msafara huo katika wilaya Manyoni ambapo aliomba kupata nao chai kabla ya kuendelea na safari ya kuelekea Burundi.

Kingu amesema kuwa amefurahishwa waandishi hao kwa kuamua kwenda Burundi kuipa sapoti timu ya taifa katika mchezo huo muhimu wa kuwania kufuzu.

“Niwapongeze kwa uzalendo huu ambao mnaufanya, kiukweli siyo jambo dogo, nipo huku kwa ajili ya ziara za kijimbo ambazo huwa nafanya siku za wikiendi lakini niliposikia mnapita nikasema nitawaona, nimefurahi na hakika mnakwenda kuwa sehemu ya historia ya nchi,” alisema Kingu

Comments are closed.