The House of Favourite Newspapers

Mfahamu Mtu Mwenye Umri Mkubwa Zaidi Duniani Aliye Hai

0

KIKONGWE Kane Tanaka ndiye mwanamke anayetambuliwa kuwa na umri mkubwa zaidi duniani aliye hai. Hii ni kulingana na kitabu cha Rekodi za Ulimwenguni za Guinness.

 

Tanaka raia wa Japan alizaliwa Januari 2, 1903. Kwa sasa ana umri wa miaka 117 na zaidi ya siku 266 mpaka leo Alhamisi.

 

Awali, Wizara ya Afya, Kazi na Ustawi wa Jamii ilisema rekodi ya nyuma ilikuwa inashikiliwa na mwanamke mwingine Mjapan, Nabi Tajima, kutoka Kisiwa cha Kikai kilicho kusini-magharibi mwa Japan, ambaye alifariki Aprili 2018.

 

Tanaka, ambaye ni mtoto wa saba miongoni mwa tisa, ni nesi katika jiji la  Fukuoka na Machi mwaka jana alitunukiwa zawadi ya kuwa binadamu mwenye umri mrefu zaidi anayeishi.

 

Mwanamke wenye umri mkubwa zaidi aliyewahi kuishi ni  Jeanne Calment wa Ufaransa aliyeishi miaka 122 na siku 164 ambapo mwanamme aliyeishi umri mkubwa zaidi alikuwa  Jiroemon Kimura  wa Japan, aliyezaliwa Aprili 19, 1897 akafariki akiwa na umri wa miaka 116 na siku 54,  siku ya Juni 12, 2013.

Leave A Reply