Mkude: Tunaanza kukusanya mataji Jumamosi

KIKOSI cha Simba, Jumamosi hii kitashuka uwanjani kupambana na Azam FC katika mchezo wa Ngao ya Jamii utakaochezwa kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

 

Hata hivyo, kiungo mkabaji wa Simba Jonas Mkude ameliambia Championi Jumatano kuwa wamejipanga vilivyo kwa ajili ya mchezo huo ambao utawafungulia ukurasa wa mataji msimu huu.

 

Alisema kwa upande wao wachezaji wapo tayari kwa mchezo huo na anaamini kabisa watafanya vizuri kama ambavyo wanatarajia ili lengo lao hilo liweze kutimia japokuwa anajua watakumbana na upinzani mkubwa kutoka kwa wachezaji wa Azam.

“Tunaendelea kujifua kwa ajili ya kujiweka fi ti tayari kwa mechi zetu zijazo ikiwemo ile ya Ngao ya Jamii dhidi ya Azam tutakayocheza Jumamosi. “Hakika tumejipanga kushinda mchezo huo ili tuweze kufungua ukurasa wetu wa mataji msimu huu kama ilivyokuwa msimu uliopita,” alisema Mkude.

 

Awali mechi hiyo ilikuwa imepangwa kupigwa kwenye Dimba la Samora mkoani Iringa lakini sasa imetangazwa kuwa itapigwa kwenye Dimba la Taifa jijini Dar es Salaam.

ZANTEL Waja na OFA Hii BAABKUBWA Kwa Wateja Wao


Loading...

Toa comment