The House of Favourite Newspapers

MKURANGA wautolea udenda mjengo wa Global

0
Nyumba iliyotolewa kwa mshindi wa Shinda Nyumba Awamu ya kwanza mwaka jana 2016.

 

WAKATI siku za kuchezeshwa kwa droo kubwa ya Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili zikikaribia, wakazi wa Mkuranga mkoani Pwani, wameimezea mate zawadi ya kwanza ambayo mshindi wake atakabidhiwa mjengo huo wenye thamani ya mamilioni ya shilingi.

 

Wakizungumza wakati walipotembelewa na timu ya promosheni ya Shinda Nyumba, wakazi hao ambao ni wasomaji wa magazeti yanayochapishwa na Global Publishers ambayo ni Ijumaa, Championi, Uwazi, Ijumaa Wikienda, Amani na Risasi, walisema wanatamani kama mshindi wa zamu hii akiwa ni mkazi kutoka Mkuranga.

 

“Mwaka jana wakati wa bahati nasibu ile ya kwanza, mshindi alitoka Iringa, sasa na sisi tunaomba angalau mwaka huu, kama sitakuwa mimi, basi awe mkazi mwingine yeyote kutoka Mkuranga ashinde hii nyumba maana kuna wasomaji wengi sana wa magazeti ya Global huku kwetu,” alisema Twaha Mjomba, ambaye alisema hajawahi kukosa gazeti za Global tangu zoezi hilo lianzishwe.

Wasomaji wakichangamkia magazeti ya Global Publishers.

 

Msomaji mwingine, Tere Misha, alisema ana matumaini makubwa ya kuibuka mshindi, maana tangu kutangazwa kwa bahati nasibu hiyo, hajawahi kukosa kununua magazeti na hajawahi kushinda hata zawadi moja katika droo ndogo zote tano zilizochezeshwa.

 

“Nimejaza kuponi nafikiri zinatosha hata kiroba, sijawahi kushinda hata kofia kwenye droo zote ndogo ambazo nilikuwa nafuatilia sana. Hiki ndicho kitu kinachonipa tumaini kubwa la kuibuka na ushindi wa nyumba katika droo kubwa inayokuja, siwezi kuwa na bahati mbaya msimu mzima nisipate kitu,” alisema Misha.

 

Juni 30 mwaka jana, Nelly Mwangosi alitangazwa kuwa mshindi wa Bahati Nasibu ya Shinda Nyumba Awamu ya Kwanza, iliyoendeshwa pia na kampuni ya uchapaji magazeti ya Global Publishers, katika droo kubwa iliyofanyika katika kwenye Viwanja vya Mbagala Zakheem jijini Dar.

 

Wasomaji wakijaza kuponi.

 

 

Tukio kama hilo, linaelekea kutokea tena mwaka huu katika Bahati Nasibu nyingine ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili ambayo droo yake kubwa itafanyika wakati wowote kuanzia sasa, ikiwa ni baada ya kuchezwa kwa droo ndogo tano, ambazo wasomaji zaidi ya 30 wamejipatia zawadi za pikipiki, televisheni, simu za kisasa za mikononi, ving’amuzi, fulana na kofia.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Yohana Mkanda, alisema jana kuwa huu ni wakati muafaka wa wasomaji wote waliokata kuponi zao kuziwasilisha kwa mawakala wao nchi nzima.

 

“Nyumba siyo kitu kidogo, kila mtu angetamani kumiliki nyumba jijini Dar es Salaam, sasa hii ni fursa adimu ambayo haikulazimu kuwa na mamilioni ya kujenga au kununua, ni kiasi cha kwenda kwa muuza magazeti yeyote, popote alipo Tanzania na kujipatia mojawapo ya magazeti yetu ili ujiweke katika nafasi nzuri ya kuwa mmoja wa wamiliki wa nyumba bora nchini,” alisema Mkanda.

 

Nyumba hiyo ambayo kama ile ya kwanza imejengwa Dar es Salaam, itakuwa ni ya kisasa ikiwa na samani zote ndani yake, kiasi cha kumfanya mshindi kuingia na begi lake tu ili kuanza maisha. Bahati Nasibu hii ya Shinda Nyumba Awamu ya Pili imedhaminiwa na Kampuni ya Premier Bet.
Afisa

NA: MWANDISHI WETU| GAZETI LA UWAZI

====

Mzungu Yamkuta Mahakamani Kisutu, Anatia Huruma

Leave A Reply