The House of Favourite Newspapers

SHINDA NYUMBA YAACHA GUMZO MKURANGA

1

 

shinda nyumba mkuranga
Nasri Ismailo wa Mkuranga akiwa katika picha ya pamoja na Mr Shinda Nyumba baada ya kujaza kuponi

Kuelekea droo kubwa ya Bahati Nasibu la Shinda Nyumba Awamu ya Pili kutoka Kampuni ya Global Publishers, wachapichashaji wa magazeti ya Champion, Uwazi, Ijumaa, Ijumaa Wikienda, Amani, na Uwazi, promosheni ya shindano hilo mwishoni mwa wiki hii imeacha gumzo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.

 

Gumzo hilo limeachwa na timu nzima ya masoko kutoka Global Publishers wakiongozwa na Mr Shinda Nyumba  punde baada ya kuwasili wilayani humo. Utitiri wa watu walikusanyika kushuhudia urefu wa Mr Shinda Nyumba huku wakinunua magazeti ya Global na kujaza kuponi sanjari na kupiga picha na Mr Shinda Nyumba.

 

Ofisa Masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroob, alipata nafasi ya kuzungumza na wakazi wa Mkuranga na kuwaasa kuendelea kuchangamkia ujazaji wa kuponi kwa kununua magazeti ya Global Publishers katika siku hizi za mwishomwisho kuelekea kilele cha shindano hilo ambapo mshindi atajinyakulia nyumba ya kisasa iliyojengwa kwa mamilioni ya shilingi. Nyumba hii, inapatikana Bunju jijini Dar es Salaam.

shinda nyumba mkuranga
Ally na Hamisi wa Mkuranga wakijaza kuponi mbele ya Mr Shinda Nyumba
shinda nyumba mkuranga
Mzee shindo (kushoto) na Khalifa, wakiwa na Mr Shinda Nyumba
shinda nyumba mkuranga
Wasomaji wa gazeti la Championi wakiendela kupata uhondo baada ya kujaza kuponi ya shindano la Shinda Nyumba
shinda nyumba mkuranga
Akina mama wajasiriamali soko kuu la Mkuranga, wakisaidiwa kujaza kuponi na ofisa masoko wa Global Publishers, Jimmy Haroub

Na: Ally Katalambula

1 Comment
  1. […] wakati walipotembelewa na timu ya promosheni ya Shinda Nyumba, wakazi hao ambao ni wasomaji wa magazeti yanayochapishwa na Global Publishers ambayo ni Ijumaa, […]

Leave A Reply