Mkwasa: Mawasiliano na Tshishimbi Yamepotea

Kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi.

WAKATI waandishi wakijaa kwenye Uwanja wa ndege wa ere, kumsubiri kiungo wa Yanga, Papy Kabamba Tshishimbi, Katibu Mkuu wa timu hiyo, Charles Mkwasa, amesema mawasiliano na staa huyo yamepotea.

Awali ilitangazwa kuwa mchezaji huyo raia wa Congo DR angetua nchini saa nane za mchana huu, lakini hadi sasa hajatua na katibu huyo amesema mwanzo walikuwa na mawasiliano naye lakini ghafla yamepotea na hawajui atatua saa ngapi.

“Sijui atatua saa ngapi, tumepoteza mawasiliano naye tukimtafuta hatumpati, hivyo kama atakuja baadaye basi tutawataarifu,” alisema Mkwasa.

 


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Loading...

Toa comment