The House of Favourite Newspapers

MREMBO ATOBOLEWA MACHO, AUAWA KIKATILI NA MPENZI

0
MREMBO ATOBOLEWA MACHO
Marehemu Maria Pius enzi za uhai wake.

KIJaNa mmoja ambaye jina lake halikufahamika mara moja, anadaiwa kumtoboa macho mpenzi wake aliyefahamika kwa jina la Maria Pius kisha kumuua kikatili na kuutupa mwili wake kichakani.

 

KISIKIE CHANZO

Taarifa za awali kutoka kwa chanzo chetu zilieleza kuwa, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Chanika jijini Dar ambapo ilidaiwa marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake uliohusisha wivu wa kimapenzi. Ilielezwa kuwa, wawili hao walikuwa wakiishi pamoja kwa muda mrefu lakini ikatokea hali ya kutoelewana hivyo kila mmoja kuwa na maisha yake.

 

“Walikuwa wakiishi mbalimbali lakini mwanaume amekuwa akimfuata Maria mara kwa mara na kutaka warudiane lakini mwisho wa siku uliibuka mzozo mkubwa ambao ulikuwa ukiishia kupigana,” kilidai chanzo. SiKu Ya tuKiO SaSa Ilielezwa, siku ya tukio mwanaume alifika nyumbani kwa Maria majira ya usiku kisha kuibua mzozo uliosababisha ugomvi mkali ikiwemo kupigana ndipo mauaji yakatokea ambapo mwili wa mrembo huyo ulikutwa ukiwa na majeraha usoni na macho yakiwa yametobolewa.

 

Akizungumzia mauaji hayo, kaka wa marehemu Maria, Edward Pius aliliambia Risasi Jumamosi kuwa, mwili wa Maria ulikutwa ukiwa na simu mbili kifuani, moja ya marehemu na nyingine ya mpenzi wake.

 

“Siku hiyo kuna mtu alikuwa akimpigia simu Maria lakini ilikuwa ikiita tu ndipo akaamua kumfuatilia nyumbani kwake na kukuta ameuawa, akatoa taarifa kwa watu kabla ya taarifa hizo kufikishwa polisi,” alisema Edward.

 

MSIBA MWANANYAMALA

Baada ya mwili wa Maria kupatikana, ulichukuliwa na Jeshi la Polisi kwa uchunguzi na Jumatano iliyopita ulichukuliwa na ndugu zake ambapo ulipelekwa nyumbani kwao Mwananyamala na kuzikwa kwenye makaburi ya Mwananyamala.

 

MAJIRANI WAZUNGUMZA, MAMA ASHINDWA!

Waandishi wetu walifika msibani Mwananyamala na kutaka kuzungumza na mama mzazi wa marehemu bila mafanikio ila baadhi ya majirani walionesha kusikitishwa na tukio.

 

“Kwa kweli tumesikitishwa mno na tukio hili kwani marehemu Maria alikuwa mtu wa watu na hata huyo bwana wake hakuwahi kuonesha ukatili wa namna hiyo, kama ni kweli yeye ndiye amemuua mkewe, basi ni ajabu sana,” alisema mmoja wa majirani wakati akizungumza na waandishi wetu.

 

Hata hivyo, taarifa zilizopatikana baadaye zilidai kuwa, mwanaume aliyetekeleza mauaji hayo naye alikutwa amekufa maeneo ya Chanika ambapo mwili wake ulipatikana ndani ya shimo la maji taka.

 

KAMANDA WA POLISI ATHIBITISHA

Akizungumza na Risasi Jumamosi kwa njia ya simu, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa Ilala, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Salum Hamduni alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema:

 

“Ni kweli tuna taarifa za mauaji hayo, ambapo maiti ya mwanamke ilipatikana Agosti 8, mwaka huu ikiwa na majeraha usoni na maiti ya mwanaume ilikutwa ikiwa kwenye shimo la maji taka siku mbili baadaye na zote tulizichukua kwa uchunguzi, lakini hatuwezi kuthibitisha kama mwanaume ndiye muuaji maana inadaiwa ni mpenzi wake, uchunguzi bado unaendelea.”

MREMBO ATOBOLEWA MACHO

IMEANDIKWA NA: BRIGHTON MASALU, ALLY KATALAMBULA NA IRENE MNYITAFU| RISASI JUMAMOSI

Leave A Reply