The House of Favourite Newspapers

Chanika Wachangamkia Ijumaa na ‘Shinda Nyumba’

1

1.Mwajuma Zuberi (katikati) akishuhudiwa na Ofisa Masoko wa Global, Yohana Mkanda (kushoto) alipokutwa akilisoma gazeti la Ijumaa.

2..Kevin Joseph maarufu kama ‘Muuza Supu’ katika stendi ya daladala  (kulia) akijaza kuponi  kushiriki bahati nasibu ya Shinda Nyumba.

3.Emmily Hassan (wa pili kushoto) akisaidiwa kujaza kuponi na Mkanda.

4Mkanda amkimsaidia Emmili kukata kuponi.

5.Msomaji wa Ijumaa aitwaye , Ezra Charles,  akijaza kuponi  ili kushiriki droo kubwa ya Shinda Nyumba.

6.Mdau mahiri wa gazeti la Ijumaa, Jonson Ndibalema (kulia) akioneshwa sehemu ya kurasa iliyo na kuponi ya bahati nasibu.Mdau mahiri wa gazeti la Ijumaa, Jonson Ndibalema (kulia) akionyeshwa sehemu ya kurasa iliyo na kuponi ya bahati nasibu.

7.Eva Jeseph mkazi wa Chanika mwisho naye akishiriki kujaza kuponi ya Shinda Nyumba.Eva Jeseph mkazi wa Chanika-Mwisho naye akishiriki kujaza kuponi ya Shinda Nyumba.

8.Mdau mahiri wa gazeti la Ijumaa, Makame Ngowi maarufu kwa jina la Marekia (katikati) akipewa maelekezo na Jimmy Haroub (kulia).Mdau mahiri wa gazeti la Ijumaa, Makame Ngowi  maarufu kwa jina la Marekia (katikati) akipewa maelekezo na Jimmy Haroub (kulia).

IKIWA ni hatua za mwisho za lala-salama ambapo zimebaki siku 12 kuchezeshwa droo kubwa ya bahati nasibu ya ‘Shinda Nyumba’  leo Ijumaa  promosheni ya shindano hilo inayoendelea iliwafikia  wakazi wa Chanika nje kidogo ya jiji la , Dar,  waliojitokeza  kwenye gari la matangazo kuchangamkia toleo Jipya la gazeti la Ijumaa ambalo ni jipya na bei mpya ya shilingi 1,000 na kushiriki kujaza kuponi za bahati nasibu.

Bahati nasibu hiyo inaendeshwa na Kampuni ya Global Publishers wachapishaji wa magazeti ya Championi, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Ijumaa Wikienda.

Maofisa masoko wa Global Publishers,Yohana Mkanda na Jimmy Haroub waliwafikia wasomaji katika mitaa mbalimbali ya maeneo ya Chanika na kuwahamasisha kushiriki bahati nasibu hiyo.

Katika uhamasishaji huo, Yohana Mkanda alirudia wito wake kwamba: “Siku zimebaki 12 nunueni magazeti ya Global mengi na mjaze kuponi ili kujiongezea nafasi ya kushinda nyumba kwani unaweza kuwa wewe au yule na kugeuka kuwa baba au mama mwenye nyumba! Kazi kwako, nyumba ndiyo hiyoo…!!!”

NA DENIS MTIMA/GPL

1 Comment
  1. […] za awali kutoka kwa chanzo chetu zilieleza kuwa, tukio hilo lilijiri mwishoni mwa wiki iliyopita, Chanika jijini Dar ambapo ilidaiwa marehemu alikuwa na ugomvi na mpenzi wake uliohusisha wivu wa kimapenzi. Ilielezwa […]

Leave A Reply