The House of Favourite Newspapers

Mrembo Kutoka Puerto Rico, Stephanie Del Valle Ashinda Taji la Miss World 2016

miss-world-2Mshindi wa Miss World 2016, Stephanie Del Valle akivishwa taji na  Miss World 2015, Mireia Lalaguna

miss-world-1

miss-world-3Stephanie Del Valle akishindwa kuamini kama kweli ameshinda Taji hilo.

MAREKANI: Mrembo kutoka Puerto Rico, Stephanie Del Valle ashinda Taji la Miss World 2016. Mrembo wa Dominican alikuwa wa pili na mrembo wa Indonesia akawa wa tatu kwenye mashindano hayo ya 66 yaliyofanyika nchini Marekani jana Jumapili.

miss-world-5

Stephanie Del Valle, katikati, baada ya kutajwa kuwa ndiye mshindi namba moja waTaji la  Miss World, Miss Philippines Catriona Elisa Gray, kushoto, na Miss Kenya Evelyn Njambi Thungu kulia.

Del Valle, 19, ana macho yabrown, ni mwanafunzi na ana uwezo wa kuzungumza Kihispania, Kiingereza na Kifaransa kwa ufasaha.

miss-world-4Akivishwa taji hilo na Mshindi wa Miss World 2015, Mireia Lalaguna wa Hispania, Del Valle amekuwa msichana wa pili kunyakuwa taji hilo nchini mwake ambapo mara ya kwanza alinyakuwa Wilnelia Merced mwaka 1975.

Miss wa Ufilipino, Catriona Elisa Gray na Miss Kenya, Evelyn Njambi pia waliingia kwenye kinyang’anyiro cha Tano Bora.

miss-world-6Baadhi  ya warembo walioshiriki mashindano hayo.

Puerto Rico imekuwa nchio ya 17 kwa kutoa washindi wengi kwenye mashindano hayo tangu yalipoanzishwa mwaka 1951. Nchi ambazo zimewahi kushinda mataji hayo zaidi ya mara moja ni kama ifuatavyo, Uingereza (5), India (5), Marekani (3), Jamaica (3), Iceland (3), ujerumani (2) na Australia (2).

Comments are closed.