The House of Favourite Newspapers

Msimu Huu wa Sikukuu, Airtel Money na WhiteBall Wazindua ‘Cheza Ushinde’

0
Meneja Mahusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusiana na ushirikiano huo. Kulia ni Meneja Mahusiano wa WhiteBall, Nasra Mohamed

 

 Wateja wa AIRTEL MONEY kupata fursa ya kujishindia pesa,simu, TV na PikiPiki

msimu huu wa sikukuu kila siku na kila wiki

28 th November, 2023

Airtel Money kwa kushirikiana na WhiteBall leo wamezindua mchezo mpya wa ‘ChezaUshinde’ maalumu kwa wateja wa Airtel Money kujishindia pesa taslimu, simu, TV na Pikipiki.

Mchezo huu wa ChezaUshinde unaopatikana kwenye menu ya Airtel Money, *150*60#,

umezinduliwa leo kama sehemu ya shamrashamra za sikukuu ili kuwapa nafasi wateja wa Airtel kushinda zawadi mbalimbali.

Akizungumza wakati wa uzinduzi, Meneja Mahusiano wa WhiteBall, Nasra Mohamed amesema mchezo huu wa ChezaUshinde ni wa kipekee kulinganisha na michezo mingine kwani unampa mteja machaguo mengi ya aina za michezo anayoweza kushiriki.

‘Mteja wa Airtel Money anaweza kuchagua kutoka kwenye zaidi ya michezo 5 iliyopo kwenye menu ili kujishindi zawadi za papo hapo, Jackpot za kila saa, kila siku na kila wiki’ alisema Nasra.

Namna ya kushiriki mchezo huu ni rahisi:

1. Bonyeza menu ya Airtel Money: *150*60#

2. Chagua namba 5: Lipia Bili

3. Chagua namba 6: Bahati Nasibu

4. Kisha Chagua namba 2: Gaming

5. Kisha Chagua namba 1: ChezaUshinde

6. Baada ya hapo unaweza kuchagua mchezo wowote kati ya michezo 5 iliyopo uweze kujishindia

7. Kushiriki ni shilingi 1,000 tu

Meneja Mahusiano wa Airtel, bwana Jackson Mmbando alisema hii ni mara ya kwanza kwa Airtel Money kuzindua mchezo wa aina hii na hivyo kuwataka wateja wa Airtel Money kuchangamkia fursa iliyotolewa.

 

‘Hii ni fursa muhimu kwa wateja wa Airtel Money kupitia msimu huu wa sikukuu kuhakikisha

wanajishindia zawadi mbalimbali kama simu,TV, pikipiki na pesa taslimu’ alisema bwana

Mmbando.

Mchezo huu umeanza rasmi hii leo na kuanzia sasa wateja wa Airtel Money wanaweza kuanza

kushiriki, kwa kuzingatia vigezo na masharti, na wawe na umri kuanzia miaka 18 na kuendelea.

Kwa maelezo zaidi: Mitandao (Facebook, Instragram):ChezaUshinde

 

Namba ya simu: 0748774400

Leave A Reply