The House of Favourite Newspapers

Mtoto wa Mwalimu Nyerere Afariki Dunia

0

FAMILIA  ya Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere imepata msiba wa mtoto wao Rosemary Nyerere aliyefariki jana jioni jijini Dar es Salaam.

 

Mmoja wa wanafamilia aliyejitambulisha kwa jina la Sophia Nyerere ameandika katika mtandao wa Instagram kuwa shangazi yake amefariki.

 

Manyerere Jacton amethibisha kuwa ndugu yao amefariki.

 

“Ni kweli dada amefariki jioni hii, lakini taarifa rasmi itatolewa,” amesema Manyerere.

Rosemary alikuwa miongoni mwa watoto saba wa Mwalimu Nyerere.

Leave A Reply