visa

MUNA AIPANGA NDOA YAKE KICHWANI!

MuigizaJi wa kitambo kwenye tasnia ya filamu Bongo, Rose alphonce ‘Muna’ amefunguka kuwa, anaiona ndoa yake siku za hivi karibuni hivyo tayari ameanza kuipanga jinsi itakavyokuwa.

Akizungumza na amani, Muna alisema kila mtu asimame kwenye maono yake na ndicho anachokisimamia na kuomba ili Mungu amtimizie maono yake juu ya ndoa yake. “Mimi hapa napanga kila kitu changu cha harusi kwa sababu mdomo wa heri unaumba vizuri na kutengeneza kila kitu hivyo Mungu ataifanya harusi yangu na itakuwa nzuri ya kupendeza na kila mmoja atasimulia utukufu wa Mungu,” alisema Muna bila kutaja kama tayari amepata mchumba au la.

Muna ambaye kwa sasa ameokoka, aliwahi kuolewa na jamaa aitwaye Peter Zacharia kisha kuachika. Pia aliwahi kutoka na mtangazaji wa Clouds TV, Casto Dickson ambaye pia walimwagana
Toa comment