The House of Favourite Newspapers

Mwakalebela Kufungua Academi ya TFF

0
Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela akizungumza na wanahari.

Katibu Mkuu wa zamani wa TFF, Frederick Mwakalebela anayegombea urais amezindua kampeni zake kwa kusema kuwa ameanzisha programu mpya ya kurudisha academy ya mpira wa miguu hapa nchini ili kukuza vipaji vya vijana wanaopenda soka.

 

“Nataka kuirudisha academy tuliyokuwa nayo TFF wakati wa Uongozi wa Leodeger Tenga na mimi nikiwa Katibu Mkuu wake enzi hizo, iliyowazaa akina Thomas Ulimwengu, Hassani Kessy ambayo hivi sasa haipo,” alisema.

Akifafanua jambo.

 

Akizungumza na wanahabari katika Hoteli ya Double View iliyopo Sinza mapambano jijini Dar, Mwakalebela amesema kuwa katika mikakati yake, amepanga kuifanya tasnia ya soka kuwa biashara kwa vijana.

 

Aidha ameeleza kuwa anafanya jitihada za kuboresha miundombinu ya mchezo huo hasa viwanja vya kuchezea ili viwe na hadhi nzuri vitakavyotumika kwa ajili ya michezo mbalimbali.

 

NA MUSA MATEJA | GLOBAL PUBLISHERS

Leave A Reply