Mwendesha Baiskeli Afariki Akikwepa Ndege

MWANAMME mmoja raia wa Australia amefariki dunia katika ajali ya baiskeli wakati akijaribu kukwepa ndege aina ya kwenzi aliyekuwa akipaa juu yake. Mwendesha baiskeli huyo mwenye umri wa miaka 76 alipata jareha  kichwani jana Jumpaili wakati alipopoteza mwelekeo kutoka barabarani na kujigonga kwenye uzio mmoja kusini mwa Sydney.

 

Licha ya jitihada za wahudumu wa afya kumuokoa, jamaa huyo alifariki alipofikishwa hospitalini baadaye. Ndege hao kwa kawaida ni tishio nchini Australia na mara nyingi husababisha majeraha kwa waendesha baiskeli na hata wapita njia, lakini, hata hivyo, ni  nadra kwa waathiriwa kufariki.

 

Polisi wamesema watawasilisha ripoti ya mpasuaji maiti baada ya tukio hilo huko Wollongong, New South Wales. Vyombo vya habari vimeripoti kwamba kumeshuhudiwa mashambulio mengine kadhaa ya ndege hao kwenzi katika bustani kulikotokea ajali hiyo.

Kwenzi wa Australia ni tofauti na ndege wa Ulaya ambao wana jina kama hilo. Wakati wa msimu wa kujamiiana, ndege hao huwa wakali na huwashambulia binaadamu wanaopita katika maeneo wanakoishi.

 

Mapema mwezi huu, serikali ya mtaa huko Sydney ilizusha mzozo wakati maofisa wa wanyama pori walipompiga risasi kwenzi mkubwa, aliyewatishia wakazi wa eneo hilo kwa miaka kadhaa. Ndege huyo mkali aliwashambulia watu kadhaa na kusababisha baadhi kujeruhiwa na kupelelekwa hospitalini.

Mkazi mmoja pia alipatwa na mshtuko wa moyo baada ya kukabiliana na ndege huyo, shirika la habari nchini Australia linaripoti. Maafisa kwa wakati huo, walitetea uamuzi wa kumuua kwenzi huyo mkubwa. Ndege huyo hulindwa kwa sheria nchini  humo lakini anaweza kudhibitiwa pia na  maafisa wa utawala.


Loading...

Toa comment