The House of Favourite Newspapers

Bwana wa Zari Afichua Siri Nzito!

DAR ES SALAAM: Mwanaume wa zamani wa mwanamama mjasiriamali, raia wa Uganda, Zarinah Hassan ‘Zari The Boss Lady’ aitwaye Robert Ogwal ‘Bob’, ameibuka na kufichua siri ya mwanamama huyo.

Bob amedai kuwa, Zari anasumbuliwa na ugonjwa wa kupaniki na kuwa na hasira za ghafla.

 

Bob anasema, moja ya matukio ya Zari anayoyakumbuka wakati wa penzi lao, ni kitendo cha kuwazaba makofi wahudumu wa hotelini (jina hakulitaja) baada ya kukasirika kufuatia kumcheleweshea oda yake ya chakula.

Bob ni miongoni mwa wanaume wanaotajwa kutoka kimapenzi na Zari.

 

Mwanaume huyo alitoka na Zari mara tu baada ya mwanamama huyo kutengana na aliyekuwa mumewe, marehemu Ivan Ssemwanga kabla ya kutua kwa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ ambaye alizaa naye watoto wawili na kutengana mwaka jana.

Bob aliueleza ulimwengu kuwa wanamuona tu Zari wa upande mmoja bila kumjua upande wa pili ni mtu wa aina gani.

 

Jamaa huyo alimtuhumu Zari ambaye ni mama wa watoto watano kuwa ni mtu mwenye hasira za hatari ambazo humsabisha kupaniki wakati wowote na mahali popote.

Kwa mujibu wa Bob, Zari huwa anajenga chuki kwa mtu yeyote anayeona anamshushia hadhi yake.

 

Bob alifikia hatua hiyo baada ya ule mjadala wa tabia aliyoionesha Zari wakati wa Shindano la Miss Uganda 2019 kwenye Hoteli ya Sheraton jijini Kampala, Uganda ya kuitwa ‘mama’ na MC Anita Fabiola kisha kuwa mbogo.

“Zari siyo mtu wa kumchezea, anaweza kukubadilikia muda wowote kama alivyofanya kwa MC Anita,” alisema Bob.

Comments are closed.