The House of Favourite Newspapers

‘NDUGU WA NEYMAR’ ATUA SINGIDA UNITED

KLABU ya Singida United, imemtangaza mshambuliaji wake mpya Felipe Olveira Dos Santos ambaye ni raia wa Brazil ambako anatokea Straiker wa PSG, Neymar Jr.
Dos Santos amewahi kuwika katika klabu ya Asec Mimosa ya nchini Ivory Coast.
Wote watatu wametambulishwa na Mkurugenzi wa Singida United, Festo Sanga wakati akizungumza na wanahabari jijini Arusha leo, wakiwa tayari kwa ajili ya Fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam (FA) watakapocheza na Mtibwa Sugar, Jumamosi hii, Juni 2, 2018 na baadaye kuelekea Kenya michuano ya SportPesa Super Cup.
Wengine wawili waliotangazwa na Singida Utd ni Amara Diaby, raia wa Ivory Coast aliyetokea Asec Mimosa,  na Tiba George John kutoka Ndanda FC.

Comments are closed.