×

Nghambi azindua kampeni kuwania Makamu Rais TFF

Mgombea wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Mulamu Nghambi(katikati) akizungumza na wanahabari.

 

MGOMBEA wa nafasi ya Makamu wa Rais wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Mulamu Nghambi, leo amezindua kampeni zake rasmi na kutaja vipaumbele vitano atakavyofanyia kazi iwapo atachaguliwa katika nafasi hiyo.

Nghambi ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Chama cha Soka Mkoa wa Dodoma (Dorefa) anawania nafasi hiyo katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Agosti 12, mwaka huu mkoani Dodoma.

Katika uzinduzi alioufanya leo jijini Dar, Nghambi ambaye amekuwa kiongozi wa soka kwa miaka 18, alisema kuwa moja ya vitu atakavyohakikisha vinakuwa sawa ni suala la ushirikiano na viongozi wengi kwa lengo la kuleta maendeleo ya mchezo huo nchini.
“Endapo nitapa nafasi hii ambayo nawania katika uchaguzi, naahidi kuwa nitaitendea haki kutokana na uzoefu nilio nao kwa kutumikia soka katika nyadhifa mbalimbali kwa kipindi cha miaka 18 sasa.

Dhamira kubwa si kuongelea uzoefu wangu ila kuweka wazi malengo yangu ya msingi yaliyonisukuma kuwania nafasi hii na ushirikiano na viongozi wenzangu, mipango ya muda mfupi na muda mrefu ambayo naamini itakuwa na faida kubwa katika kukuza soka letu,” alisema Nghambi.

 

NA DENIS MTIMA/GPL

Leave a Comment