NECTA Yatangaza matokeo ya Darasa la Nne na Kidato cha Pili, Yapo Hapa – Video

Baraza la Mitihani la Taifa (NECTA) Januari 10, 2026 limetangaza matokeo ya upimaji wa kitaifa wa Darasa la Nne na Kidato cha Pili.
Matokeo hayo yametangazwa na Katibu Mtendaji wa NECTA, Prof. Said Mohamed katika Ofisi za Baraza la Mitihani jijini Dar es Salaam.
Prof. Mohamed amesema jumla ya wanafunzi 1,324,970 kati ya 1,490,314 wenye matokeo, sawa na asilimia 88.91 wamefaulu kuendelea na darasa la tano kwa mwaka 2026 ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 2.67.
Ameongeza kuwa wanafunzi 705,091 kati ya 811,074, sawa na asilimia 86.93 wamefaulu kuendelea na kidato cha tatu ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia 1.52 ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2024.
BONYEZA LINK HIZI CHINI

MATOKEO YA UPIMAJI WA KITAIFA WA DARASA LA NNE (SFNA) 2025