The House of Favourite Newspapers

Neymar Aumia, Azua Hofu PSG

KUFUATIA nyota wa PSG ya Ufaransa, Neymar Jr kuumia wakati wa mchezo wa Ligi Kuu ya Ufaransa kati ya timu yake dhidi ya Marseille, jana usiku, kipa wa PSG, Alphonse Areola amesema anawasiwasi na kuumia kwa mshambuliaji huyo.

 

PSG iliibuka na mabao 3-0, Neymar alitolewa kwa Machela baada ya kuumia kifundo cha mguu huku akiacha hofu kama atakuwa tayari kurejea dimbani kabla ya mchezo wa marudiano Kombe la UEFA dhidi ya Real Madrid Machi 6.

 

“Nina wasiwasi juu ya Neymar, niliona alivyoumia mguu wake na ulivimba hapohapo,” amesema Areola. Golikipa huyo ameongeza kuwa Neymar ni mchezaji muhimu kwenye timu hivyo wana matumaini atarejea hivi karibuni.

 

Aidha, ocha wa PSG, Unai Emery amesema Neymar atapona kabla ya marudiano na Madrid ambao utapigwa kwenye uwanja wa Parc des Princes. PSG inaongoza ligi ikiwa na alama 71, tofuati ya pointi 14 na timu inayoshika nafasi ya pili Monaco yenye alama 57, huku Marseille ikiwa katika nafasi ya tatu na alama 55.

Comments are closed.