The House of Favourite Newspapers

NUH MZIWANDA ALIA NA MASHABIKI WAKE

0

NUH MZIWANDA ALIA

 

NUH MZIWANDA ALIA…

‘STRESS’ za kumwagana na aliyekuwa mke wake ambaye pia ni mzazi mwenziye, zinaendelea kuutesa ubongo wa mwanamuziki wa Bongo fleva, Nuh Mziwanda, ambapo hivi karibuni ameamua kuomba ushauri kwa mashabiki wake, juu ya mwanamke gani atamfaa katika maisha yake.
Nuh ambaye ni baba wa mtoto mmoja aliyezaa na aliyekuwa mkewe, Nawal, akiwa kwa sasa ni mke wa mwanaume mwingine anayeitwa Masoud, ametumia mtandao wa kijamii wa Instagram, kuwaomba ushauri mashabiki wake.

Nimejifunza mengi sana kwenye ‘life style’ yangu ya kimapenzi na najitoaga sana, ila siku ya mwisho naumizwa, je unahisi mwanamke wa aina gani atanifaa na nitaweza kudumu naye? Leo nawaachieni mashabiki wangu mmalize hili,” ameandika Nuh.

NUH MZIWANDA ALIA
Baada ya posti hiyo, baadhi ya mashabiki wake walitoa maoni tofautitofauti.

Pole wapo waliotulia wengi, ila tuliza akili wakati wa kufanya maamuzi

“Usioe Mzee mpaka miaka ifike 60, tafuta mapene

Muoe Ebitoke

We naye kajinga tu hao wote uliopita nao kama haujapata wa kukufaa sisi tukikuchagulia ndiyo atakufaa tatizo unafanya vitu kwa mihemuko ndugu yangu kama bado akili yako haijakomaa kuishi na mwanamke acha kwanza pengine uzeeni utaweza

Hizo ni baadhi ya komenti za ushauri wa mashabiki wa Nuh Mziwanda, zinazopatikana katika posti yake .

NA ISRI MOHAMED/GPL

Leave A Reply