P DIDDY ADAIWA ‘KUNYAKUWA ’ DOGODOGO

KACHAFUKA! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya mkongwe kwenye gemu la Muziki wa Hip Hop kutoka Marekani, Sean John Combs ‘P Diddy’ kudaiwa kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na binti mdogo, Lori Harvey ambaye ni mtoto wa mtangazaji maarufu nchini Marekani, Steve Harvey.

Kwa muda mrefu kumekuwa na tetesi kwa P Diddy (49) na Lori Harvey (22) wanatoka kimapenzi na haikuwa imethibitishwa lakini juzi kati mrembo huyo alionekana akipiga misele na gari la P Diddy aina ya Chauffeured Maybach jambo ambalo hakuwahi kulifanya.

Inadaiwa P Diddy, tayari ameshamvalisha pete ya uchumba bibiye huyo ambaye alishawahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mtoto wake, Justin Combs.

Toa comment