The House of Favourite Newspapers

Polepole Atinga Yanga, Atoa Milioni Moja

WAKATI jana Yanga wakifanya uchaguzi wao wa kuwachagua viongozi wapya wa klabu hiyo, Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Humphrey Polepole alikuwa miongoni mwao ambapo alitoa kiasi cha shilingi milioni moja ikiwa ni sehemu ya mchango wa timu hiyo.

 

Polepole alihudhuria uchaguzi huo wa Yanga ambao ulifanyika katika Ukumbi wa Bwalo la Polisi, Oysterbay jijini Dar ambapo wanachama wa klabu hiyo walipata nafasi ya kuchagua mwenyekiti, makamu mwenyekiti na wajumbe wa kamati ya utendaji.

 

Kiongozi huyo wakati akizungumza na wanachama ambao walikuwa ukumbini hapo, alisema: “Hii ni nafasi kwenu wanachama wa Yanga kuchagua viongozi ambao watatuongoza kwa kipindi kijacho. Ni muhimu zaidi kuwachagua wale ambao wataleta maendeleo katika klabu hii kwa kipindi kijacho cha uongozi, msije mkafanya makosa.

 

“Nitatoa kiasi cha shilingi milioni moja ambacho kitasaidia katika michango ambayo inaendeshwa na timu katika kujiendesha kwake.”

Sweetbert Lukonge na Said Ally, Dar es Salaam

POLEPOLE: YANGA SC Haita Shuka Ninguvu Moja

Comments are closed.