POSHY HAACHI UMACHINGA KAMWE

Jacqueline Obeid ‘Poshy’

MREMBO aliyejipatia jina kutokana na umbo lake, Jacqueline Obeid ‘Poshy’ ameibuka na kusema kuwa kamwe hawezi kuacha umachinga anaofanya kisa amepata umaarufu.

 

Poshy aliliambia Gazeti la Ijumaa kuwa kipindi cha nyuma alipokuwa chuo alikuwa akifanya biashara zake za kuuza mikanda na nguo mbalimbali za kike na kiume na anaendelea nayo mpaka sasa na hafikirii kuiacha.

“Kuna watu wananiuliza ninawezaje kumpelekea mtu mzigo popote alipo wakati sasa hivi nimekuwa maarufu yaani jina langu ni kubwa, nimekuwa nikiwashangaa na kuwajibu kuwa jina kubwa bila kuwa na kipato chochote ni kazi bure kwa hiyo umachinga sitauacha kamwe maana ni kazi inayonilipa,” alisema Poshy.

Stori: Imelda Mtema

WEMA SEPETU ”SITAKI Kushauriwa Kwenye Mapenzi”Amtaja Moze Iyobo


Loading...

Toa comment