Povu la Jay Z Lamchanganya Benet, Aposti Tena
JAY Z si mtu wa mchezomchezo. Si unajua kipindi cha nyuma msela ambaye anaimba muziki wa RnB, Eric Benet alimdisi Jay Z kwamba alioa mwanamke msagaji, sasa ili kuonyesha kwamba alikuwa bega kwa bega na mama watoto wake, Jay Z akaamua kumchana msela kwenye ngoma yake ya Kill Jay Z kwa kuimba mstari huu “You almost went Eric Benet, Let the baddest girl in the world get away, I don’t even know what else to say. Ni–a, never go Eric Benet!”
Benet alivyoona kwamba amechanwa, hakutaka kuremba, hapohapo akaweka posti iliyosomeka ‘Hey yo #Jayz! Just so ya know, I got the baddest girl in the world as my wife….like right now!’ kuonyesha kwamba mistari imemuingia ingawa anajifanya kama kupotezea hivi kiasi fulani.
Kumbuka kwamba leo Jay Z ameachia albamu yake ya 4:44 ambayo imeanza kuuzwa katika mtandao wake wa Tidal.
Na: Nyemo Chilongani, GPL