visa

Pretty Kind: Nimekoma Kupenda Wanaume wa Nje

YAMEMKUTA! Msanii wa filamu na muziki Bongo, Suzan Michael ‘Pretty Kind’ ameibuka na kusema kuwa amekoma kupenda wanaume wa nje ya nchi. 

Akipiga stori na Showbiz Xtra, Pretty alisema baada ya kupata mpenzi ambaye raia wa Nigeria alimuahidi kumuoa ambapo alikuja Bongo lakini alimtaka amposti kwenye mitandao ya kijamii naye kukataa ikawa ndiyo sababu ya penzi kuvunjika.

“Nilimpata mchumba wa Nigeria lakini tumeachana kisa nimekataa kumposti kwenye mitandao ya kijamii maana naona alitaka umaarufu kupitia mimi, baada ya kukataa penzi likaishia hapo, nimekoma kupenda wanaume wa nje,” alisema Pretty.

 

Kwa upande mwingine aliwataka warembo kuwa makini kwani wanaume wa nje hasa wanaopatikana mitandaoni siyo wazuri wana lengo la kuwatumia kwa manufaa yao na mwisho wanaenda kuoa wanawake wa huko kwao.
Toa comment