The House of Favourite Newspapers

PROF JAY AMPA HESHIMA MONDI

Joseph Haule ‘Professor J’

MSANII wa muziki wa Bongo Fleva, Joseph Haule ‘Professor J’ ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Mikumi mkoani Morogoro, juzikati alivutiwa na ngoma mpya ya Diamond Platnumz inayoitwa Inama aliyomshirikisha mwanamuziki Fally Ipupa.

 

Kuonesha kuwa alivutiwa na kibao hicho, Professor J alikisifia na kumueleza Diamond kuwa ni ‘muvi’ la kikubwa sana kisha akamwambia anamheshimu.

 

“Respect Chibu hii ni muvi la kikubwa,” aliandika mwanamuziki huyo kwenye ukurasa wake wa Instagram. Diamond kwenye wimbo huo amewataja watoto wake ambao anadai kuwa mapenzi yamesababisha ugomvi mpaka anaishia kuwaona mtandaoni na ku-like picha zao.

Comments are closed.