The House of Favourite Newspapers

Sheria ya Makosa ya Mtandao Yamkamatisha Mhandisi Mzungu (VIDEO)

1
…Akimkazia jicho paparazi wa Global Publishers.

RAIA wa Afrika Kusini ambaye ni mhandisi, Menelaos Tsampos, leo amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kwa kosa la kumtishia mtu kwa njia ya mtandao kupitia mfumo wa kompyuta.
Akiwasilisha kesi hiyo, wakili wa serikali, Nassoro Katuga, amemsomea raia huyo mashtaka manne mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi, Cyprian Mkeha.

 

Mshitakiwa Menelaos Tsampos akikwepa kamera za mapaparazi mahakamani.

Katuga amedai Juni 22, mwaka huu maeneo ya jijini Dar es Salaam, kupitia mfumo wa kompyuta alituma ujumbe wa baruapepe (E-mail) uliokuwa na maneno ya vitisho kwa mtu anayeitwa Costa Gianna, ikiwa ni kinyume na sheria ya mtandao kifungu cha 23(1) na (2) namba 14 ya mwaka 2015.

 

…Akiwa kizimbani.

Pia inadaiwa kwamba Julai 20, mwaka huu alimtishia tena mtu huyo kupitia baruapele yake, ambapo alimwambia anampa saa 48 ili watatue mgogoro baina yao kinyume na hapo angemfanyia kitu kibaya.
Katuga amedai kosa jingine ni kuishi nchi bila kibali na kukutwa na hati ya kughushi ya kusafiria ambapo aliyatenda makosa hayo kati ya Julai na Agosti mwaka huu jijini Dar.

…Akiwa kizimbani.

 

Baada ya kusomewa makosa hayo, mshtakiwa aliyakana makossa hayo na wakili wa serikali aliiomba mahakama imnyime dhamana mshtakiwa kutokana na uhalisia wa makosa aliyoyafanya ambapo, hata hivyo, wakili wa utetezi, Jebrah Kambole, alidai makosa hayo yanadhaminika.
Hakimu Mkeha ameahirisha kesi hiyo hadi Agosti 16, mwaka huu na akaamuru mshtakiwa huyo akaguliwe Viza na makazi yake.

NA DENIS MTIMA/GPL

 

LIVE: Mapokezi ya Rais Abdel Fattah El-Sisi wa Mirsi Ikulu -Dar

1 Comment
  1. […] kosa hilo katika kipindi hicho kwa lengo la kujaribu kujipatia fedha kwa njia ya udanganyifu. Mshtakiwa alikana shitaka na upande wa mashtaka ulidai upelelezi bado […]

Leave A Reply