The House of Favourite Newspapers

Rais Putin: Nimeimarisha Uhusiano Wangu na Trump

0
Rais wa Urusi, Vladmir Putin, akisalimiana na Rais wa Marekani,  Donald Trump.

RAIS wa Urusi, Vladmir Putin,  amesema kuwa ameimarisha ushirikiano wake wa kikazi na rais wa Marekani Donald Trump ambapo amesema kuwa kufuatia mkutano wake na rais huyo ana kila sababu ya wawili hao kuweka kiwango cha ushirikiano kinachohitajika.

Kiongozi huyo wa Urusi alisema kuwa usitishwaji wa mapigano kusini mwa Syria uliotangazwa hapo jana unatokana na kile alichokitaja kuwa msimamo wa ushirikiano mzuri na Marekani aliposisitiza kwamba rais huyo wa Marekani yuko tofauti sana katika maisha ya kawaida kuliko anavyoonekana katika runinga .

Pia amesema kuwa anaamini kwamba  Trump amekubali hakikisho lake kwamba Moscow haikuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka uliopita.

Leave A Reply