Rais Samia Ahesabiwa Sensa Ikulu Chamwino Dodoma, Atoa Ujumbe kwa Watanzania -Video
RAIS Samia leo Jumanne, Agosti 23, 2022 amekuwa miongoni mwa Watanzania waliohesabiwa katika Sensa ya Watu na Makazi iliyoanza saa 6:01 usiku.
Mkurugenzi Mkuu wa ofisi ya Takwimu Tanzania (NBS), Albina Chuwa na Kamishna wa Sensa ya Watu na Makazi mwaka 2022, Anne Makinda wameongoza timu kwenda Ikulu ya Chamwino, Mkoa wa Dodoma kwa ajili ya kumhesabu Rais Samia.
Mara baada ya kumaliza kumhesabu, kazi iliyodumu si zaidi ya nusu saa, Rais Samia amezungumza na waandishi wa habari akisema, “nimemaliza kuhesabiwa, ni kweli maswali ni mengi kidogo lakini yanajibika, ombi langu kwa wananchi ni kuweka taarifa zetu mapema.”
Rais Samia amemaliza kuzungumza kwa kusema, “niitakie nchi yetu sensa njema, makarani wetu wafanyekazi kwa ufanisi na wananchi wajitokeze kutoa majawabu yanayotakiwa.”