Rais Samia Awachana Ma-RC Na Ma-DC Wanaotaka Ubunge – Video
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan leo Machi 11, 2025 amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri, Wakuu wa Wilaya na viongozi wengine wa serikali za mitaa kutangaza mapema nia yao ya kugombea ubunge katika uchaguzi mkuu wa Oktoba 2025.
Akizungumza jijini Dodoma katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa 39 wa ALAT, Rais Samia amesema hatua hiyo inalenga kuhakikisha nafasi zao zinajazwa na watu wenye sifa mapema, huku akiwaonya dhidi ya kushtukiza wakati wa uchaguzi.
“Watakaoshindwa kusema mapema, ipo hatihati ya kukosa yote. Lakini wale watakaotoa taarifa mapema, ikiwa watashindwa, bado kuna nafasi ya kurejeshwa serikalini,” amesema Rais Samia.
Amesisitiza kuwa uchaguzi si bahati nasibu, bali unapaswa kuwa na watu makini wenye dhamira

