The House of Favourite Newspapers

RATIBA YA SEHEMU UTAKAPOPITA MWILI WA DR. MENGI KESHO HII HAPA

Mwili wa aliyekuwa Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Dr.Reginald Mengi unatarajiwa kupokelewa kesho, ambapo utaletwa kwa ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kutokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiararabu.

 

Mwili wake utaletwa na ndege ya Shirika la Ndege la Emirates kutokea Dubai, Umoja wa Falme za Kiarabu (U.A.E) majira ya saa 8:00 mchana.

 

Baada ya mwili kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa JNIA, utapitishwa maeneo ya Tazara, Buguruni, Ilala, Kigogo, Magomeni na Kinondoni.

 

Kutoka Kinondoni, mwili wake utapitishwa hadi Morocco, barabara ya Bagamoyo, Sayansi, Mwenge hadi katika hospitali ya Lugalo ambako mwili wa Dr. Reginald Mengi utahifadhiwa.

 

Ratiba hiyo itaendelea siku ya Jumanne ya Mei 7, 2019, ambapo mwili utapelekwa katika ukumbi wa Karimjee, kwa ajili ya watu wote kuuaga na kisha utarejeshwa nyumbani kwake.

Siku ya Jumatano mwili utasafirishwa kupelekwa Moshi Machame ambako Ibada ya mazishi itafanyika siku ya Alhamis katika kanisa la Kisereni (KKKT).

Comments are closed.