The House of Favourite Newspapers

RC PAUL MAKONDA AKABIDHIWA KOMBE LA SIMBA (PICHA +VIDEO)

MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda akikabidhiwa kombe na Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems makao makuu ya Simba, mitaa ya Msimbazi, Kariakoo.

PAUL Makonda, mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam, leo amekuwa mgeni rasmi kwenye shughuli za kuwapokea mabingwa wa Ligi Kuu Bara Simba, msimu wa 2018/19 mitaa ya Msimbazi,Kariakoo.

Wachezaji wa Simba wakiwa juu ya gari lililo wazi wakiwaonyesha kombe mashabiki wao, mitaa ya Msimbazi,Kariakoo

Mabingwa hao mara mbili mfululizo wamerejea leo wakitokea Morogoro ambapo walikuwa na mchezo wa mwisho jana uwanja wa Jamhuri na Mtibwa Sugar.

Makonda amekabidhiwa kombe hilo na nahodha msaidizi wa Simba, Mohamed Hussein pamoja na kocha mkuu wa kikosi hicho, Patrick Aussems.

Comments are closed.