ROMY ETI KAMWE ‘HAMCHITI’ MKEWE

KAKA wa mwanamuziki maarufu Nasibu Abdul ‘Diamond’, Romeo Jones ‘Romy Jons’ amefunguka kuwa katika kitu ambacho hawezi kukifanya ni kumsaliti mke wake kwani anampenda sana hivyo kufanya hivyo kutamuuma sana. 

 

Romy alisema kuwa, huko nyuma angeweza kusema anahangaika kwa vile ujana unamsumbua lakini kwa sasa hivi ametulia sana na anamuomba Mungu kila kukicha amlindie ndoa yake.

 

“Kitu ambacho namuomba Mungu siku zote shetani tu asiniingie nikamsaliti mke wangu maana hiyo itaniumiza sana kwa sababu nampenda na sitaki kumkosea kwa dhambi ya usaliti hata kidogo,” alisema Romy.

 

Romy alifunga ndoa na mkewe Kahuye Jord ‘Kay Jord’, Desemba 1 mwaka 2017 ambapo baadaye aliangusha bonge la sherehe katika Ukumbi wa Cardinal Rugambwa maeneo ya Oysterbay jijini Dar na kuhudhuriwa na mastaa kibao.

Stori: Imelda Mtema


Loading...

Toa comment