The House of Favourite Newspapers

ROSE NDAUKA AFUATA NYAYO ZA WEMA, UWOYA!

MWANAMAMA kutoka Bongo Movies, Rose Ndauka amefuata nyayo za warembo wenzake, Wema Sepetu na Irene Uwoya kwa kujikita kwenye ujasiriamali. Mrembo huyo amesema kutokana na hali jinsi ilivyo na soko la sinema kusuasua, ameaona ni vyema kujiongeza kwa kufungua saluni inayojishu-ghulisha na usafi wa mwili kwa watu wote.

“Hii itakuwa ni sehemu ya usafi kuanzia watoto, wanaume na wanawake inaitwa Connexion Unisex House of Beuty hapa Sinza-Africa Sana (Dar),” alisema Rose wakati akiizindua saluni hiyo hivi karibuni. Wema na Irene walimtangulia mrembo huyo kwa kujishughulisha na ujasiriamali ambapo Wema ana duka la nguo za watoto huku Uwoya akiwa na baa.

Comments are closed.