The House of Favourite Newspapers

ROSE NDAUKA: KUIGIZA MAISHA ‘KUMEEKSIPAYA’

Rose Ndauka

MSANII wa filamu za Kibongo, Rose Ndauka amesema kuwa kitu kikubwa kilichopitwa na wakati ‘kueksipaya’ kwa mastaa ni kuigiza maisha kwa sababu hata hizo pesa za kuigizia hakuna.  Akizungumza na Ijumaa Wikienda, Rose alisema kama kuna staa anahangaika na kuigiza maisha atakuwa anachelewa sana kufanya vitu vyake maishani mwisho wake atapotelea kwenye kuigiza siku zote.

“Mambo ya kuigiza na kufeki maisha yalipitwa na wakati, tuigize tu hivi hivi michezo yetu na si vitu vingine maana zamani hata hela za kuigizia zilikuwepo, sio sasa hivi,” alisema Rose Ndauka.

Comments are closed.