The House of Favourite Newspapers

Ruby: Simchukii Nandy

0
Ruby.

MWANAMUZIKI wa Bongo Fleva, Hellen George ‘Ruby’ ameibuka na kueleza kuwa hafikirii wala hajawahi kumchukia msanii mwenzake, Faustina Charles `Nandy’ kama watu wengi wanavyozusha mitandaoni.

Ruby aliiambia Risasi Vibes kuwa amekuwa akisikia watu wakizungumza mengi kwamba anamchukia Nandy kwa kuwa eti anafanya vizuri kwenye muziki kuliko yeye, jambo ambalo siyo kweli kwani hamchukii na mara nyingi huwa anapenda kuimba nyimbo zake.

Nandy.

“Simchukii Nandy kama watu wanavyosema, namuombea mafanikio na atimize ndoto zake, kuhusu muziki ni hivi, sifanyi muziki wa mashindano kwa sababu kila mtu amepewa kitu chake cha tofauti na Mungu, kwani najua wanaweza wakaja kina Nandy wengine na hawawezi kuwa yeye wala mimi, nafanya kazi nzuri kwa ajili ya kufika mbali na siyo kwa ajili ya mashindano,” alisema Ruby.

 

Gladness Mallya | RISASI MCHANGANYIKO

Leave A Reply