SAJENTI: NGUO FUPI HAZIMHARIBU MTOTO

MUIGIZAJI Husna Idd ‘Sajenti’ amesema kitendo cha yeye kumvalisha mwanaye nguo fupi hakimaanishi kwamba mwanaye ataharibikiwa kitabia. 

 

Sajenti amesema, kwenye mitandao ya kijamii watu wamekuwa wakimsema kwamba anamharibu motto kwa kumvalisha nguo fupi kama ambavyo yeye anavaa, jambo ambalo si kweli.

“Nguo fupi sio kigezo cha motto kuharibikiwa kitabia, inategemea tu wewe kama mzazi unamfundisha nini mwanao au namleaje.

 

Kwangu mimi sioni tatizo, anavaa nguo fupi na bado mwanangu ana maadili mazuri kwani namfundisha hivyo,” alisema Sajenti ambaye alizaa mtoto huyo na mwanamuziki wa Bendi ya The African Stars ‘Twanga Pepeta’, Charles Gabriel ‘Chaz Baba’


Loading...

Toa comment