The House of Favourite Newspapers

Sheva Apewa Ulinzi Maalum Simba

MSHAMBULIAJI wa Simba, Miraji Athuman ‘Sheva’ amepewa ulinzi maalumu ndani ya Simba ambao utamwezesha kuwa katika afya nzuri muda wote.

 

Hatua hiyo, imekuja baada ya mchezaji huyo hivi karibuni kukosekana katika mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Prisons ambayo Simba ilishindwa kupata ushindi baada ya kusumbuliwa na maumivu ya mwili.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, mmoja wa viongozi wa benchi la ufundi la Simba ambaye ameomba hifadhi ya jina lake, alisema kuwa hivi sasa Sheva pamoja na wachezaji wengine, wamepewa ulinzi maalumu. “Tunaendelea vizuri na maandalizi yetu katika kipindi hiki ambacho ligi imesimama kupisha mechi ya timu ya taifa.

“Lakini jambo kubwa ambalo kwa sasa lipo kikosini kwetu ni mkakati kabambe kuhusiana na wachezaji, kwani hivi sasa wamepewa ulinzi mkubwa wa afya zao. “Madaktari wametakiwa kufanya kazi yao ipasavyo ili kila mchezaji awe fiti muda wote.

 

Kukosekana kwa Sheva katika mechi yetu na Prisons lilikuwa ni pigo kwani pengine angekuwepo tungepata ushindi kutokana na aina ya uchezaji wake,” alisema kiongozi huyo.

 

Alipoulizwa kuhusiana na hilo, Kocha Mkuu wa Simba, Patrick Aussems alisema: “Afya za wachezaji ni jambo muhimu sana kwangu, kwani unapokuwa na majeruhi wengi timu itakumbana na changamoto nyingi uwanjani kwa hiyo ni lazima tuwe makini kuhakikisha wanakuwa fiti muda wote.

Comments are closed.